Tamu Chungu Ya Ripoti IPCC

By Jenifer Julius
IPCC ni jopo la kiserikali la kimataifa, linalofanya kazi ya kutathmini mabadiliko ya hali ya hewa kidunia, jopo hili lina mchango mkubwa katika mwenendo wa mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuwa ripoti inayotolewa na jopo hili ndio inayoleta majadiliano ya namna ya kukabiliana na janga hili.Jopo hili linatoa tathmini ya athari ya mabadiliko ya hali ya hewa kila baada ya miaka mitano au pale inapohitajika kulingana na matakwa ya Umoja wa Mataifa.Ripoti inayojadiliwa hivi sasa katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi unaoendelea jijini Bonn, inahusu athari za ongezeko la nyuzi joto ya nyuzi  1.5 katika maendeleo endelevu kidunia.Majadiliano haya yanahusu ni nini ripoti inazunguza ni kwa vipi jumuia ya Umoja wa Mataifa na nchi na nchi mbalimbali zinaweza kuitumia kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi katika nyanja ya kupunguza hewa chafu na jinsi ya kuzuia athari hizo.Hoja kuu inayojadiliwa katika ripoti hiyo ni ifikapo mwaka 2030 kama jitihada za kutosha hazitofanyika, joto la dunia litaongezeka hadi kufikia nyuzi 1.5, ambayo itakuwa na athari kubwa katika sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii duniani.Inendelea kusema kuwa kama hali ikiendelea kuwa kama ilivyo ifikapo mwaka 2052 joto la dunia litafuikia nyuzi 2.Ambayo itakuwa na athari kubwa zaidi.Moja ya athari za moja kwa moja zinazotegemea kutokea ni kupungua kwa uzalisahaji katika sekta ya kilimo lakini vile vile kutoweka kwa viumbe wa baharini (mikoko)hasa yale ya majani kufikia 70% hadi 90% kufikia mwaka 2030 endapo joto hilo litakuwa limeongezeka kufikia nyuzi joto 1.5 na kama ikifika nyuzi joto 2 asilimia 99 wa viumbebahari watapotea.Na hali hii inaweza kusababisha kupotea kwa viumbe hai wa baharini kama vile samaki kwa na kuathiri sekta ya uvuvi.Hali ilivyoHata hivyo baadhi ya nchi hasa zilizoendelea kama vile Soud Arabia, Marekani, quwait na nyinginezo hazijakubaliana na ripoti hiyo zikijenga hoja kuwa hii kuna baadhi ya mambo ambayo hayakufanyiwa kazi na hayakuzungumzwa .Pia wanahoji kuwa imetokana na vyanzo vichache na kuna baadhi ya vipengele havijafanyiwa utafiti kabisa katika ripoti hii kahivyo wanataka mataifa yasitilie mkazo ripoti hii na wasubiri zijazo.Hata hivyo nchi nyingi zinaunga mkono  ripoti hii kwa kuona kuwa inajitosheleza na inafaa kutumika katika utekelezaji wa kupambana athari za mabadiliko ya tabia nchi hasa katika kipengele cha kupunguza hewa chafu na kujikinga na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Hoja ya pili ikilenga kuwa hii ni ripoti maalum na bado kuna ripoti maalum kuu mbili zinakuja kabla ya kutoka ripoti kuu ambayo itatoa sasa tathmini ya hali ya mabadiliko ya haliya hewa kwa hiyo yale ambayo hayaguswa au kufanyiwa kazi yatatekelezwa kwenye ripoti zinazokuja. Maoni ya wadauDkt. Ranslaus chang’a, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa  kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa ambaye ndio  ndio muendeshaji mkuu wa mjadala huu, anasema Tanzania  imefurahishwa na kazi kubwa iliyofanywa na jopo hili katika ripoti hii.Anaongeza kuwa Tanzania ikifuata muongozo wa ripoti hiyo basi itafanikiwa kuzuia athari za mabadiliko ya hali ya hewa ikiwamo kuzuia joto kuongezeka.“ Naweza kusema kuwa tayari tunafanya utekelezaji wa hii ripoti kwa sababu tumeweka kipaumbele  kuhakikisha tunazuia  tunasafisha hewa chafu, kama unavyoona Sera ya mazingira imejikita katika kudhibi na kupunguza athri za mabadiliko ya tabia nchi.“Tumeweka kupaumbele upandaji miti, tunawaelimisha wakulima kuhusu kujikinga na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na mengine mengi” anasema Dkt. Stanslaus.
Mariam Inam, Ofisa mawasiliano kutoka shirika la kimataifa la WWF nchini Pakistan anasema anaikubali ripoti IPCC kwa sababu inaonyesha athari za joto la dunia kufikia nyzi 1.5  hivyo ni jukumu la nchi kuifuata au la.“Nimefurahi pia kuona imeongelea kujikita katika njia za kisayansi kukabiliana na mabadilio ya tabia nchi kwa kuwa nchi yangu inahitaji kufuata njia hizo”, anasema Mariam.Profesa msaidizi katika chuo kikuu cha Hokkaido nchini japan, Tomohito Yamada, anasema wanaitumia mbinu mbalimbali zilizoelekezwa katika ripoti hiyo nchini kwao kuzuia athari za mabadiliko ya tabia nchi.“ japan, hasa kijijini kwetu tunapata mafuriko ya mara kwa mara pale mvua itakaponyesha , na sisi kama kitengo kinachohushiana na mazingira tutaitumia ripoti hiyo, inamsaada mkubwa,” alisema YamadaNaye mwenyekiti wa bodi ya sayansi na techonojia ( subsidiary body for scientifical and techological advice) katika mkutano huo wa mabadiliko ya tabia nchi  SBSTA, kutoka nchini Paris, Paul Watkinson, anasema japokuwa ripoti hiyo ina upungufu mwingi lakini imetoa muongozo mzuri ambao  unafaa kwa nchi zinazoendelea kuutumia kujikinga na athari za mabadiliko ya tabia nchi.Chini ya mkataba wa NDC uliopo ndani ya Makubaliano ya Paris, mataifa yamekubaliana kupeleka ripoti ni ya mipango wanayofanya ili kupunguza hewa chafu kila nchi kwa wakati wake lakini mwisho wa mwaka huu wataweka muda maalum wa kuandaa ripoti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Copyright © The African Pages 2020.All rights reserved.