Nafasi Ya Wanawake Kwenye Vita Dhidi Ya Mabadiliko Ya Tabianchi

CREDIT: Jenifer Julius
 Mabadiliko ya tabianchi (climate change)  yanayotokana na kuongezeka kwa kiwango cha joto la dunia, yanaendelea kuleta athari kubwa duniani.Kunapotokea majanga yanayotokana na athari za kama vile; kimbunga, mafuriko, joto, na ukame, waathirika wakuu ni watoto na wanawake.
Ripoti ya mwaka 2018 iliyotolewa na shirika linalohudumia wanawake (UN Women) inaonyesha kuwa  athari za mabadiliko ya Tabianchi zinawaumiza kwa kiasi kikubwa wanawake na watoto kwa kuwa uwezekano wa kundi hili kufa kutokana na athari hizi ni mara 14 ukilinganisha na wanaume.Mfano mzuri ukionekana nchini Tanzania hasa sehemu za vijijini jinsi wanawake wanavyotumia muda mwingi na kutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.Katika kijiji cha kilole kata ya kwamngumi baadhi ya wanawake hutumia masaa ma tatu kuteka maji kutokana na umbali uliopo kutoka nyumbani hadi kwenye mabomba ya maji.Katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea jijini Bonn, nchini Ujerumani, unaojadili mikakati ya kufikia Makubaliano ya Paris ya kupunguza kiwango cha joto kufikia nyuzi mbili, moja ya mijadala inayoendelea ni umuhimu wa kuwajumuisha wanawake katika mkakati huu.
Mashirika kutoka sehemu mbalimbali kama vile Action AidUn women , walifanya kongamano lililolenga umuhimu  ni wa kuhusisha wanawake katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na ni kwa vipi itawezekana.Kuwajumuisha wanawake katika madawati yanayohusisha na vita dhidi ya madiliko ya tabia nchi ni moja ya mambo yanajadiliwa kwa dhana ya kwamba wanawake wana mawazo yanayopelekwa kutoa suluhisho juu ya athari hizi kama wakipewa nafasi.Hoja hiyo imejengwa na dhana kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zinawakumba wanawake moja kwa moja hivyo wao ndio wanamajibu sahihi ya nini kifanyike ili kukabiliana hali hii.
Kuwaingiza wanawake katika miradi yenye lengo la kupunguza  ongezeko la joto kama vile kuwaonyesha fursa za kibiashara, ikiaminika kuwa wanawake wana mzigo kubwa wa kubeba familia na hivyo wakipewa fursa hizi watazitekeleza ipasavyo ili kuweza kusaidia familia zao.Kwa mamtiki hiyo lengo la kufikia Makubaliano ya Paris litafikiwa kwa urahisi kama wanawake wakipewa nafasi ya kuchangia .
Kiongozi wa harakati za  Mabadiliko ya Tabianchi kutoka shirika la Kimataifa Christian aid, Mohamed adoe anatoa mawazo yake akisema kuwa njia nyingine ni kufanya uhamasishaji wa vijana wa kike na kuwapa fursa za kujifuza na kufahamu zaidi mabadiliko ya tabia nchi kupitia, workshop, kutengeneza wanaharakati wa mapambano dhidi ya ongezeko la joto ili wakue na uelewa huo.Nchi kama Ujerumani vijana wanapewa msaada kutoka mashirika mbalimbali wanapotaka kuishinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya athari ya mabadiliko ya tabia nchi.Baadhi ya mifano hai inayopaswa kuigwa na nchi zinazoendeleaSerikali na mashirika ya siyo ya kiserikali yanatakiwa kutoa msaada kusaidia vikundi vya kinamama vinavyojishughulisha na teknolojia yenye lengo la kudhibiti ongezeka la joto kama vile miradi ya umeme jua, majiko ya gesi, kaboni n,k.Hii inatakiwa iende sambamba na kutambulisha teknolojia inayolenga kuwa mbadala wa visababishi vya mbadala wa ongezeko la joto duniani  pamoja na kuwaonyesha wanawake fursa zinazopatikana kutokana na teknolojia hizo.Kuweka usawa wa kimajukumu linapokuja kati ya mwanamke na mwanamume, kwamba wanawake na wanaume wakae kiti kimoja na kufanya maamuzi ya pamoja ni nini kifanyike ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.Mara nyingi inapokuja suala la kufanya maamuzi makubwa ya kujenga nchi wanawake wamekuwa wakiwekwa wakitengwa ilhali wana mengi ya kuchangia.Mwezi mei mwaka huu serikali kupitia wizara ya mambo ya nje nchini Australia imepeleka wanawake 13 kutoka bara la Asia kuhudhulia kongamano la siku tatu  wa mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni kujifunza mambo yatajadiliwa katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaendelea jiji Bonn,German. Hii yote ni kuwawezesha wanawake na kuwaingiza ulimwengu wa mambambano dhidi ya ongezeko la mabadiliko ya tabianchi nchi ili na wao waweze kutoa mchango wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Copyright © The African Pages 2020.All rights reserved.